Muhtasari
Read the full fact sheet- Ugonjwa wa mfadhaiko baada ya kiwewe (PTSD) ni mlolongo wa miitikio inayoweza kutokea kwa watu ambao wamepitia au kushuhudia tukio la kutisha ambalo linatishia maisha au usalama wao (au maisha na usalama wa watu wengine wa karibu yao).
On this page
Ugonjwa wa mfadhaiko baada ya kiwewe (PTSD) ni mlolongo wa miitikio inayoweza kutokea kwa watu ambao wamepitia au kushuhudia tukio la kutisha ambalo linatishia maisha au usalama wao (au maisha na usalama wa watu wengine wa karibu yao). Hii inaweza kuwa ajali ya gari au ajali nyingine mbaya, kushambuliwa kimwili au kingono, uhalifu, matukio yanayohusiana na vita au mateso, au maafa ya asili kama vile moto wa msituni au mafuriko. Takriban kila mtu anayepitia kiwewe zina athari za baada ya kiwewe. Lakini kwa watu wengine, athari hizi huwa hazipungui ndani ya siku chache au wiki chache, lakini zinaendelea na kutatiza maisha yao - wakati huu ndipo athari huitwa ugonjwa wa mfadhaiko wa baada ya kiwewe.
Dalili za PTSD
Mtu aliye na PTSD ana aina nne kuu za matatizo:
- Kuishi tena katika tukio la kiwewe kupitia kumbukumbu zisizotakiwa na zinazojirudia, matukio ya nyuma au ndoto za kutisha. Kunaweza kuwa na miitikio mikali ya kihisia au ya kimwili anapokumbushwa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutokwa na jasho, mapigo ya moyo au hofu.
- Kuepuka vikumbusho vya tukio husika, kama vile mawazo, hisia, watu, mahali, shughuli au hali zinazorudisha kumbukumbu za tukio.
- Mabadiliko mabaya katika hisia na mawazo, kama vile kuhisi hasira, hofu, hatia, kukata tamaa au kufa ganzi, kukuza imani kama vile kujiona "Mimi ni mbaya" au "Dunia si salama", na kuhisi kutengwa na wengine.
- Kuwa katika hali ya macho ya juu au ‘kusumbuka’ kukijionyesha kwa ugumu wa kusinzia, hasira, kukosa umakini, kushtuka kwa urahisi na kuwa macho kila mara kutokana na dalili za hatari.
Kama mtu amepitia matukio mengine ya kutisha mapema katika maisha yake, wakati mwingine hupata matukio haya ya zamani yanajitokeza na yanahitaji kushughulikiwa pia.
Mtaalamu wa afya anaweza kutambua PTSD ikiwa mtu ana dalili katika kila moja ya maeneo haya manne kwa mwezi au zaidi, ambayo husababisha shida kubwa, au huathiri uwezo wao wa kufanya kazi na kujifunza, mahusiano yao na maisha ya kila siku.
Watu walio na PTSD wanaweza pia kuwa na kile kinachoitwa 'uzoefu wa kujisikia kutengwa', ambao mara nyingi hufafanuliwa kama:
- "Ilikuwa kama vile sikuwepo pale."
- "Muda ulikuwa kama vile umesimama."
- "Nilihisi kama nilikuwa nikitazama mambo yakitokea kutoka juu."
Wakati wa kutafuta msaada kwa ajili ya PTSD
Mtu ambaye amepata tukio la kiwewe anapaswa kutafuta msaada wa kitaalamu ikiwa kama:
- hawajisikii kuwa vinaanza kuwa afadhali baada ya wiki mbili
- kuhisi wasiwasi au kufadhaika sana
- wanakuwa na athari kutokana na tukio la kiwewe ambalo linaingilia nyumbani, kazini na/au mahusiano
- wanafikiria kujidhuru wao wenyewe au mtu mwingine.
Baadhi ya ishara ambazo tatizo linaweza kujitokeza ni kama:
- kuwa mkali kila wakati au kukasirika
- kuwa na ugumu wa kufanya kazi nyumbani au kazini
- kutokuwa na uwezo wa kujibu wengine kihisia
- kuwa na shughuli nyingi isivyo kawaida ili kuepusha baadhi ya masuala
- kutumia pombe, dawa za kulevya au kucheza kamari ili kukabiliana na hali hiyo
- kuwa na matatizo makubwa ya usingizi.
Msaada ni muhimu ili kupona
Watu wengi hupata baadhi ya dalili za PTSD katika wiki mbili za kwanza baada ya tukio linalosababisha kiwewe, lakini wengi hupona wao wenyewe au kwa usaidizi wa familia na marafiki. Kwa sababu hii, matibabu rasmi ya PTSD kwa kawaida hayaanzi kwa angalau wiki mbili au zaidi baada ya tukio la kiwewe, isipokuwa mtu ahisi kufadhaishwa sana na tukio hilo.
Ni muhimu katika siku na wiki chache za kwanza baada ya tukio la kutisha kupata msaada wowote unaohitajika. Hii inaweza kujumuisha kupata taarifa, watu na nyenzo, ikiwa ni pamoja na wataalamu waliofunzwa, ambayo inaweza kukusaidia kupata nafuu. Usaidizi kutoka kwa familia na marafiki unaweza kuwa ndio kitu pekee unachohitajika. Vinginevyo, daktari ni mahali pazuri pa kuanza kupata msaada zaidi. Kitu kingine ambacho kinaweza kusaidia ni kuzungumza na wengine waliohusika katika tukio au ambao wamepitia mambo kama hayo.
Matibabu ya PTSD
Ikiwa bado una matatizo baada ya wiki mbili, daktari au mtaalamu wa afya ya akili anaweza kujadili matibabu. Matibabu madhubuti yanapatikana kwa ajili ya PTSD. Mengi yanahusisha matibabu ya kisaikolojia kama vile ushauri nasaha, lakini dawa pia inaweza kusaidia. Kwa ujumla, ni bora kuanza na matibabu ya kisaikolojia badala ya kutumia dawa kama suluhisho la kwanza na la pekee kwa tatizo hilo.
Matibabu ya PTSD huenda yakahusisha kukabiliana na kumbukumbu ya kiwewe na kufanya kazi kupitia mawazo na imani zinazohusiana na uzoefu. Matibabu yanayolenga kutibu tatizo la kiwewe yanaweza:
- kupunguza dalili za PTSD
- kupunguza wasiwasi na unyogovu
- kuboresha ubora wa maisha ya mtu
- kuwa na ufanisi kwa watu ambao wamepata matukio ya kiwewe ya muda mrefu au ya kurudia, lakini matibabu yanaweza kuhitajika kwa muda mrefu.
Mahali pa kupata msaada
- GP wako (daktari), mtaalamu wa afya ya akili, kama vile daktari wa akili, mwanasaikolojia, mshauri au mfanyakazi wa kijamii.
- Kituo chako cha afya cha jamii kilicho karibu nawe
- Huduma ya Rufaa ya Jumuiya ya Kisaikolojia ya Australia Simu. 1800 333 497
- Phoenix Australia Kituo cha Afya ya Akili baada ya Kupata Tatizo la Kiwewe Simu. (03) 9035 5599
- Centre for Grief and Bereavement (Kituo cha Huzuni na Msiba) Simu. 1800 642 066
Huduma za ushauri wa simu za jumla zinaweza kutoa ushauri:
- Lifeline Simu. 13 11 14
- GriefLine Simu. 1300 845 745
- Beyondblue Simu. 1300 22 4636
- Muuguzi wa kwenye simu Simu. 1300 60 60 24 – kwa maelezo ya afya ya kitaalamu na ushauri (saa 24, siku 7)
Kwa taarifa zaidi tembelea: